TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA – Jeshi la Zimamoto
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mamlaka aliyopewa Kwa mujibu wa kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 5(1) ya kanuni za Utumishi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za mwaka 2008 anatangaza nafasi za ajira ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vijana wenye sifa zifuatazo: –
1. Wenye elimu ya kidato cha Nne Sita za mwombaji.
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
- Awe na cheti cha kuzaliwa
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA)
- Awe na afya njema kimwili na kiakili
- Asiwe na Kumbukumbu za Uhalifu
- Awe hajaoa au kuolewa
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (Tatoos)
- Awe hajawahi kutumia aina yoyote ya madawa ya kulevya
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
- Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
- Awe mwenye urefu usiopungua futi 5.7 kwa mwanaume na futi 5.4
kwa mwanamke
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
m) Umri kuanzia miaka 18 hadi 25
- Wenye elimu ya kidato cha nne au sita ambao wana ujuzi wa udereva wa magari makubwa, Utundi bomba, Uuguzi, taaluma ya Zimamoto na Uokoaji, Utabibu na Urubani wa Helikopta.
Sita za mwombaji.
- Sifa zote zilizoainishwakwenye Aya ya 1 (a hadi m)
- Marubani wa Helikopta umri kuanzia miaka 18 hadi 35
- Madereva, awe na leseni daraja E na umri kuanzia miaka 18 hadi 28 (watakaoitwa kwenye Usaili watafanyiwa uhakiki kwa njia ya vitendo, kuendesha magari makubwa)
3. Wenye Shahada.
Uhandisi Bahari (Marine engineering), TEHAMA, Uhandisi wa Ndege (Aircraft maintenance engineers), Lugha (Kingereza), Ukadiriaji Majenzi (QS), Teknolojia ya habari (Multi-media technology), Uchumi, Sheria (waliohitimu shule ya sheria kwa vitendo), Ualimu (Education management), Usafirishaji Barabara na Reli (Road & railways transport logistics management) na Uhandisi Kemikali (Chemical processing engineering).
Sita za mwombaji.
- Sifa zote zilizoainishwa kwenye Aya ya 1 (a hadi I)
- Umri kuanzia miaka 18 hadi 28
4. Namna ya kufanya maombi.
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kikoa cha ajira.zimamoto.go.tz mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28 Februari, 2025.
Mwombaji aambatishe kwenye mfumo nyaraka zifuatazo: –
- Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono
- Nakaia ya cheti cha kuzaliwa
- Fomu ya uthibitisho wa siha njema kutoka kwa mganga wa serikali
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA
- Picha ya Pasipoti ya hivi karibuni
- Namba ya mtihani wa Kidato cha Nne
- Namba ya mtihani wa Kidato cha Sita
- Nakala ya vyeti vya kuhitimu elimu ya shahada au taaluma kutoka vyuo
vinavyotambulika na Serikali
- Barua ya Utambulisho kutoka kwa Afisa mt€ nda ji wa Kijiji/mtaa
NB:
- Nakala za vyeti zithibitishwe na Kamishna wa viapo au Hak.imu
- Barua zitakaz.owasilishwa kwa njia ya posta, mkono au kwa barua pepe
hazitapokelewa
- Waombaji wote waandike namba za simu kwenye barua zao za maombi
- Mwombaji atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uwongo atachukuliwa hatua za kisheria.