Analisiti Mwandamizi wa Mikopo (Nafasi 2) – Senior Credit Analyst
Mahali pa Kazi: Ofisi Kuu
Lengo la Kazi:
Kufanya tathmini kwa wakati na yenye ubora ya mapendekezo ya mikopo (mpya na/au iliyopo) kwa kuzingatia misingi bora ya mikopo na kifedha ili kutoa maoni ya kitaalamu kwa mamlaka za idhini ili waweze kufanya uamuzi/mamuzi sahihi.
Majukumu Makuu:
- Kutoa tathmini ya moja kwa moja (ya kitaalamu/maalamu) ya iwapo pendekezo la mkopo linakidhi vigezo na kama hatari ya mkopo kwa mshirika ipo katika viwango vinavyokubalika na kupendekeza ipasavyo pendekezo la mkopo likiwemo masharti pale inapohitajika kuweka ulinzi wa udhamini.
- Kuhudhuria na kuwasilisha hoja kwenye vikao vya Kamati ya Mikopo ya Rejareja na Kamati ya Mikopo ya Jumla.
- Kuandaa na kuwasilisha ripoti mbalimbali za mikopo kama itakavyohitajika kwenye kamati mbalimbali.
- Kuchunguza taarifa zilizopatikana ili kupata uelewa wa kina juu ya mambo ya biashara yanayosababisha faida/thamani pamoja na hatari husika.
- Kutambua, kukadiria, na kutathmini vyanzo vya hatari ya mkopo katika kikasha cha mkopo au kwa mteja mmoja mmoja na pale inapowezekana, kutoa mikakati ya kupunguza hatari.
- Kutoa msaada wa kiufundi kwa Analisiti wengine wa Mikopo/maafisa wa Mikopo, Maafisa Uhusiano/Meneja Uhusiano ikiwa ni pamoja na kuwafundisha ili kuboresha ubora wa mapendekezo ya mikopo yanayopendekezwa kuidhinishwa.
- Kuweka muundo sahihi wa dili kulingana na matumizi na mapato ya fedha.
- Kupitia maombi yaliyopitiwa na Analisiti wa Mikopo kabla ya kuwasilishwa kwa ajili ya idhini.
- Kuzingatia muda uliokubaliwa wa utekelezaji (TAT) na ratiba za CREDCO (Rejareja na Jumla) bila kuathiri ubora wa mapendekezo/maamuzi ya mikopo.
- Kuhudhuria vikao vya CREDCO (Jumla na Rejareja) vinavyofanyika kila wiki na kutoa maoni thabiti ya kimikopo na kifedha kwa mamlaka za idhini kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.
- Kuhudhuria vikao vingine vinavyohusiana na mikopo kutoka Kanda na vitengo vingine vya biashara.
- Kupitia sera ya mikopo na nyaraka husika na kufanya maboresho inapohitajika.
- Kutumia taarifa za sekta na soko zilizopo kutambua na kuelewa vitisho vinavyoweza kujitokeza kwa wateja waliopo na wapya.
- Kujenga uhusiano mzuri wa kikazi na upande wa biashara Makao Makuu na matawi ili kuboresha ubora wa mapendekezo ya biashara na muda wa kufanya tathmini za mikopo.
- Kugundua na kutathmini mabadiliko katika vipengele muhimu vya hatari kwenye uhusiano wa kibiashara au sekta na kuchambua athari za mabadiliko hayo kwenye mahusiano ya biashara yanayoendelea.
- Kufanya kazi kwa ukaribu na idara ya Hatari ya Mikopo ili kufuata matakwa ya tathmini za Hatari na Udhibiti (RCA) na mapitio mengine ya robo mwaka kama inavyotakiwa na BOT.
- Kuchukua na/au kupendekeza hatua za kurekebisha pale zilipopatikana dosari katika ukaguzi wa mikopo.
- Kuwa mlezi, kutoa mwongozo na kufuatilia Analisiti wa Mikopo kwa ajili ya tathmini za wakati na ubora wa mapendekezo yaliyowasilishwa (mapya/ya zamani).
- Kuhifadhi kumbukumbu zote za maombi ya mikopo yanayoingia na kutoka/memo nk.
- Kujibu maswali yote ya ukaguzi na yale ya BOT inapohitajika.
- Fursa za kazi kwa njia ya mtandao zipo.
Maarifa na Ujuzi:
- Uelewa wa biashara katika sekta mbalimbali: Serikali/Mashirika ya Umma, viwanda, biashara jumla, biashara ya kilimo, na rejareja.
- Uwezo wa kutetea maamuzi yake bila kuathiri mahusiano ya kibiashara.
- Uelewa wa hali ya juu wa mikopo na hatari zinazohusiana nayo.
- Uwezo ulio thibitishwa wa uhusiano mzuri wa kazi katika mazingira ya Biashara au Mikopo.
- Ujuzi wa bidhaa za mikopo ya benki.
- Ujuzi wa kina wa mbinu za uchambuzi wa mikopo.
- Uwezo wa kuchambua na kufanya mahesabu.
- Uwezo wa mawasiliano na uwasilishaji.
- Uwezo wa kufanya majadiliano.
Sifa na Uzoefu:
- Shahada ya kwanza ya Biashara/Uchumi/Fedha/Au fani nyingine zinazohusiana.
- Angalau uzoefu wa miaka 5 katika uchambuzi wa mikopo kwa maombi ya mikopo ya kampuni na SME ikiwemo mikopo ya kilimo, fedha za biashara, fedha za miradi na kadhalika.
NMB Bank Plc ni Mwajiri Mwenye Fursa Sawa Kwa Wote. Tumejikita katika kujenga mazingira ya utofauti na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika wafanyakazi. Wanawake na watu wenye ulemavu wanahimizwa sana kutuma maombi ya nafasi hii.
NMB Bank Plc haigombi ada yoyote kwenye mchakato wa kuomba au ajira. Kama utapata ombi la ulipaji wa ada, tafadhali puuza.
Ni waombaji waliofanikiwa tu ndio watakaowasiliana.
Tarehe ya kufungua maombi: 23-Apr-2025
Tarehe ya kufunga maombi: 07-May-2025