Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime anayofuraha kuwatangazia nafasi Nne (04) za kazi katika Ajira ya kudumu kwa Watanzania wote wenye sifa stahiki baada ya kupokea Kibali cha Ajira mpya kwa Mwaka 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora.
1.0 MPISHI DARAJA LA II NAFASI MBILI (02)
1.1 KAZI NA MAJUKUMU:
- Kusafisha jiko.
- Kupika chakula cha kawaida.
- Kupika vyakula vya aina mbalimbali.
- Kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula viko safi.
- Kusafisha maeneo ya kupikia.
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha IV.
- Awe amefuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya ‘Food Production’ yatolewayo na vyuo vya forodhani (Dar es Salaam), Masoka (Moshi), Arusha Hotel, VETA (Mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
1.1.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara wa Serikali Mpishi Daraja la II ataanza na TGS C kwa mwezi.
1.2 DEREVA DARAJA LA II NAFASI MBILI (02)
1.2.1 KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na msimamizi wake.
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI:
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha IV.
- Awe na leseni ya udereva ya Daraja la “C” au “E” ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali, pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yatolewayo na chuo cha VETA au NIT au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
1.2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya mshahara wa Serikali Dereva Daraja la II ataanza na TGS B kwa mwezi.
2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
- Mwombaji awe hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote la jinai.
- Waombaji wote waambatanishe nakala za vyeti vya taaluma, nakala ya cheti cha kidato cha Nne/Sita, zilizothibitishwa na Hakimu au Wakili aliyetambulika na Serikali.
- Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa iliyothibitishwa na Hakimu au Wakili anayetambulika na Serikali.
- Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu na picha moja ya passport size ya hivi karibuni (iandikwe majina kamili kwa nyuma).
- Testimonials, Provisional Results Slips, Statements of results, Hati za Matokeo za kidato cha nne na Sita (Form IV na VI Results Slips) na Transcripts ambayo haikuambatanishwa na cheti havitakubaliwa.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA au NACTE).
- Waombaji ambao ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliopo katika Utumishi wa Umma wasiombe nafasi hizi.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa sababu yeyote ile hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
- Waombaji watakaowasilisha vyeti na taarifa za kugushi watachukuliwa hatua kali za Kisheria na mamlaka zinazohusika.
- Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja II wenye Leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatanisha vyeti vya mafunzo vya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Waombaji wote waambatanishe nakala ya Kitambulisho cha NIDA au Namba ya utambulisho wa Uraia (National Identification Number) kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
- Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 11/08/2025.
- Barua zote za maombi ziandikwe kwa anuani ifuatayo:Mkurugenzi wa Mji, Halmashauri ya Mji, S.L.P 45, TARIME
- Maombi yatumwe kupitia mfumo wa Ajira Portal Tovuti www.ajira.go.tz
Imetolewa na
MKURUGENZI WA MJI TARIME
Ofisi:
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji, 7 Barabara ya Utawala, S.L.P 45, 31482 TARIME Simu Na.: +255 28 2690218 Nukushi: +255 28 2690218 Barua pepe: td@tarimetc.go.tz Unapojibu tafadhali taja: Kumb.Na. HMT/E.1/33/125