Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nanyumbu
Utangulizi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kupitia kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 chenye nafasi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (4) na nafasi ya Dereva Daraja II (5) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo:
1.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (Nafasi 04)
1.1 Majukumu ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi
1.2 Sifa za Mombaaji
- Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six)
- Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili
- Kufuzu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika
- Kuwa na ujuzi wa kutumia programu za kompyuta za ofisi kama: Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
1.3 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C1
2.0 Dereva Daraja la II (Nafasi 05)
2.1 Majukumu ya Dereva Daraja la II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
- Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako
2.2 Sifa za Mombaaji
- Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI)
- Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari
- Experience ya kazi ya angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali
- Vyeti vya mafunzo ambayo vinatoa sifa ya kupata madaraja husika
- Mahudhurio ya mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali
2.3 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B1
3.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji Kazi
- Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha ulemavu wao kwenye Mfumo wa kuombea ajira
- Waombaji waambatise maelezo binafsi (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani, namba za simu na barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika
- Maombi yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ikiwemo vyeti vya Kidato cha Nne au Sita na vyeti vya mafunzo mbalimbali
- “Testimonial“, “Provisional Results“, “Statement of results“ na hati za matokeo ya Kidato cha Nne na Sita (Form IV and VI Results Slips) HAVITAKUBALIWA
- Waombaji wa kazi za Dereva waambatise vyeti vya mafunzo na leseni husika
- Waombaji waliostaafu katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba kazi bila kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi
- Waombaji waliopo katika Utumishi wa Umma wasiendeleze kuomba kazi ila kama wanapata kibali maalum
- Kuwasilishwa kwa taarifa na sifa za kughushi kutachukuliwa hatua za kisheria
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/8/2025
4.0 Jinsi ya Kuomba
- Maombi ya kazi yatumwe pamoja na barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa, vyeti vya elimu, na anuani kwa: MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU, S.L.P 246, NANYUMBU – MTWARA
- Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani: https://portal.ajira.go.tz/
- Maombi yanayotumwa nje ya utaratibu huu hayatatafikiwa
Imetolewa na:
Ibrahim J. Mwanauta Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU 02-08-2025