Akihutubia katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika mjini Singida, Rais Samia Suluhu Hassan amesema,
“Kwa kuwa mcheza kwao hutunzwa, mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyppanda na umepanda kwa sababu ya nguvu zenu wafanyalazi, Ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba, katika kuleta ustawi kwa wafanyakazi, mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1. Wafanyakazi hoyee!
Nyomgeza hii itakayoanza kutumika Julai Mwaka huu, itaongeza kima cha mshahara kutoka Sh370,000 hadi Sh500,000. Ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu.
Kwa upande wa sekta binafsi, bodi ya kima cha chini kwa sekta binafsi inaendelea kufanya maptio ili kuboresha viwango vya chini vya mshahara ili kuboresha sekta hiyo.”