Table of Contents
Chuo cha Centre for Foreign Relations (CFR) kilichopo Dar es Salaam, Tanzania, ni moja ya taasisi za elimu ya juu zinazojulikana kwa kutoa mafunzo ya Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa. Chuo hiki kimejipatia heshima kubwa katika kutoa elimu yenye ubora na inayolenga kuandaa wataalamu wenye ujuzi unaohitajika katika masuala ya kimataifa.
Sifa za kujiunga na chuo hiki ni muongozo muhimu unaolenga kuwasaidia wanafunzi kuelewa vigezo na taratibu za udahili ili kutimiza ndoto zao za kusomea programu zilizopo katika chuo hiki. Vigezo hivi vinasaidia kuhakikisha kwamba wanafunzi waliojiunga wana uwezo na sifa zinazohitajika kuendana na masomo ya chuo kikuu na ukuaji wa kitaaluma .
Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Shahada ya Kwanza katika CFR
Kwa waombaji wa shahada ya kwanza katika Centre for Foreign Relations, vigezo vyake ni kama ifuatavyo:
- Bachelor Degree in International Relations and Diplomacy: Waombaji wanahitaji kuwa na diploma katika Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia, Uchumi, Biashara, Sheria, Uandishi wa Habari, au masomo yanayohusiana na hayo. Wanafunzi wanatakiwa kuwa na wastani wa “B” au GPA ya chini kabisa ya 3.0.
- Bachelor Degree in Governance and Strategic Leadership: Waombaji wanatakiwa kuwa na diploma katika Utawala wa Umma, Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia, Uongozi wa Kistratejia, au masomo mengine yanayohusiana. Wanafunzi wanapaswa kuwa na wastani wa “B” au GPA ya chini ya 3.0.
Sifa na Vigezo vya Jumla kwa Kwa waombaji wa kidato cha sita (General Minimum Entry Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kabla ya 2014 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
2 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita mnamo 2014 na 2015 | Passi mbili kuu (‘C’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 kutoka kwa masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1; E = 0.5) |
3 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kuanzia 2016 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
Sifa na Vigezo vya Jumla Kwa waombaji wa Diploma (For Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waombaji wa Stashahada ya Kawaida, FTC na Sawa | Angalau pasi nne (“D” na zaidi) katika “O” Level au NVA Level III na chini ya pasi nne “O” Level au sawa na sifa za kigeni kama ilivyothibitishwa na NECTA au NACTVET; na i) Angalau GPA ya 3.0 kwa Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6); au ii) Wastani wa alama “C” kwa Cheti cha Fundi Kamili (FTC) (ambapo A=5, B=4, C=3, na D=2); au iii) Wastani wa alama “B” kwa Stashahada ya Elimu ya Ualimu; au iv) Wastani wa alama “B” kwa tuzo zinazohusiana na Afya kama Tiba ya Kliniki na nyinginezo; au v) Alama ya Heshima kwa Stashahada na vyeti visivyofungamana na NTA; au vi) Upper Second Class kwa stashahada zisizo za NTA. |
2 | Cheti cha Msingi cha OUT | GPA ya 3.0 iliyokusanywa kutokana na masomo sita muhimu na angalau Alama ya “C” kutoka masomo matatu katika klusta husika (Sanaa, Sayansi na Masomo ya Biashara) pamoja na Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari kilicho na alama angalau 1.5 kutoka masomo mawili; au Stashahada ya Kawaida kutoka taasisi inayotambuliwa yenye GPA ya angalau 2.0 AU NTA level 5 / Cheti cha Fundi wa Kitaalam Kiwango cha II. |
Taarifa kamili zaidi na sifa za kujiunga katika programu mbalimbali zinapatikana katika “TCU Guidebooks” ambayo waombaji wanaweza kupakua kupitia tovuti ya TCU kwa linki hii: TCU Guidebooks.
1 Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Uzamili na Uzamivu katika CFR
Kwa wale wanaotaka kujiunga na programu za uzamili na uzamivu, vigezo vya kujiunga ni pamoja na:
- Shahada ya Kwanza: Wanafunzi wanatakiwa kuwa na shahada ya kwanza yenye GPA ya chini ya 2.7 au wastani wa “B”.
- Uzoefu wa kazi: Programu fulani zinaweza kuhitaji uzoefu wa kazi kama kigezo cha ziada.
- PhD: Waombaji wa PhD wanahitaji kuwa na shahada ya uzamili katika fani inayohusiana na kuwa na uwezo wa kufanya utafiti unaokubalika kitaaluma.
Sifa na vigezo vya Kujiunga kwa Programu Zote
S/N | Kuingia katika | Sifa za Kuingia |
1 | Programu ya Cheti cha Uzamili | Angalau Shahada ya Kwanza (UQF level 8). |
2 | Programu ya Stashahada ya Uzamili | Cheti cha Uzamili AU Shahada ya Kwanza (UQF level 8) yenye GPA ya angalau 2.0 au alama ya C. |
3 | Programu ya Shahada ya Uzamili (aina zote) | a) Shahada ya Kwanza ya Kitaaluma inayofaa (UQF level 8) au sawa na hiyo yenye GPA ya 2.7 au alama ya B; b) Stashahada ya Uzamili katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B; au c) Sifa ya mafunzo ya kitaalam yenye mafunzo ya ziada yanayofaa, ushahidi wa uwezo wa utafiti na uzoefu wa kazi unaofaa. |
4 | Programu ya PhD (aina zote) | Shahada ya Uzamili (UQF level 9) katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B. |
Ni muhimu kwa waombaji wote kuhakikisha kuwa wanakidhi vigezo vya msingi na wanajiandaa vema kwa ajili ya mchakato wa maombi yao. Ufuatiliaji wa mwongozo wa udahili wa TCU na kutumia taarifa zilizowekwa rasmi na chuo ni njia bora ya kuhakikisha kuwa haufanyi makosa katika mchakato. Muhimu zaidi, ni lazima kujiandaa vyema na kuwa na nyaraka zote muhimu zinazohitajika kwa maombi.