Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI) kilichopo Hombolo, Dodoma, ni taasisi ya elimu ya juu inayojikita katika kutoa mafunzo ya utawala na usimamizi wa serikali za mitaa. Chuo hiki kimekuwa mstari wa mbele katika kuandaa wataalamu wenye ujuzi na maarifa ya kusimamia maendeleo ya jamii na utawala bora katika ngazi za serikali za mitaa nchini Tanzania.
Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Shahada ya Kwanza katika LGTI
Kwa waombaji wa programu za shahada ya kwanza katika LGTI, sifa za msingi zinazohitajika ni kama ifuatavyo:
- Kwa Wanafunzi Waliohitimu Kidato cha Sita (ACSEE): Waombaji wanapaswa kuwa na alama mbili za ‘Principal Pass’ katika masomo yafuatayo: Biolojia, Kemia, Fizikia, Jiografia, Kilimo, Lishe, Hisabati ya Juu, Biashara, Uchumi, Historia, Uhasibu, Lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Jumla ya alama za kuingilia ni 4.0.
- Kwa Wanafunzi Walio na Diploma au Sifa Sawa na Hizo: Waombaji wanapaswa kuwa na Diploma inayohusiana na programu wanayoomba, ikiwa na wastani wa alama ya ‘B’ au GPA ya chini ya 3.0.
Sifa na Vigezo vya Jumla kwa Kwa waombaji wa kidato cha sita (General Minimum Entry Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kabla ya 2014 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
2 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita mnamo 2014 na 2015 | Passi mbili kuu (‘C’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 kutoka kwa masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1; E = 0.5) |
3 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kuanzia 2016 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
Sifa na Vigezo vya Jumla Kwa waombaji wa Diploma (For Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waombaji wa Stashahada ya Kawaida, FTC na Sawa | Angalau pasi nne (“D” na zaidi) katika “O” Level au NVA Level III na chini ya pasi nne “O” Level au sawa na sifa za kigeni kama ilivyothibitishwa na NECTA au NACTVET; na i) Angalau GPA ya 3.0 kwa Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6); au ii) Wastani wa alama “C” kwa Cheti cha Fundi Kamili (FTC) (ambapo A=5, B=4, C=3, na D=2); au iii) Wastani wa alama “B” kwa Stashahada ya Elimu ya Ualimu; au iv) Wastani wa alama “B” kwa tuzo zinazohusiana na Afya kama Tiba ya Kliniki na nyinginezo; au v) Alama ya Heshima kwa Stashahada na vyeti visivyofungamana na NTA; au vi) Upper Second Class kwa stashahada zisizo za NTA. |
2 | Cheti cha Msingi cha OUT | GPA ya 3.0 iliyokusanywa kutokana na masomo sita muhimu na angalau Alama ya “C” kutoka masomo matatu katika klusta husika (Sanaa, Sayansi na Masomo ya Biashara) pamoja na Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari kilicho na alama angalau 1.5 kutoka masomo mawili; au Stashahada ya Kawaida kutoka taasisi inayotambuliwa yenye GPA ya angalau 2.0 AU NTA level 5 / Cheti cha Fundi wa Kitaalam Kiwango cha II. |
Sifa za Kujiunga na Programu Maalum za Shahada ya Kwanza katika Chuo cha LGTI
Chuo cha LGTI kinatoa programu mbalimbali za shahada ya kwanza, kila moja ikiwa na mahitaji maalum ya kujiunga. Hapa chini ni baadhi ya programu hizo na sifa zake:
1. Shahada ya Kwanza katika Utawala na Usimamizi wa Serikali za Mitaa
- Sifa za Kujiunga: Alama mbili za ‘Principal Pass’ katika masomo yaliyotajwa hapo juu.
- Uwezo wa Kupokea Wanafunzi: Chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 100 kwa programu hii.
- Muda wa Programu: Miaka 3.
2. Shahada ya Kwanza katika Maendeleo ya Jamii
- Sifa za Kujiunga: Alama mbili za ‘Principal Pass’ katika masomo yaliyotajwa hapo juu.
- Uwezo wa Kupokea Wanafunzi: Chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 50 kwa programu hii.
- Muda wa Programu: Miaka 3.
3. Shahada ya Kwanza katika Usimamizi wa Rasilimali Watu
- Sifa za Kujiunga: Alama mbili za ‘Principal Pass’ katika masomo yaliyotajwa hapo juu.
- Uwezo wa Kupokea Wanafunzi: Chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 50 kwa programu hii.
- Muda wa Programu: Miaka 3.
4. Shahada ya Kwanza katika Uhasibu na Fedha
- Sifa za Kujiunga: Alama mbili za ‘Principal Pass’ katika masomo yaliyotajwa hapo juu.
- Uwezo wa Kupokea Wanafunzi: Chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 100 kwa programu hii.
- Muda wa Programu: Miaka 3.
Sifa za Kujiunga na Programu za Cheti na Diploma katika LGTI
Kwa waombaji wa programu za cheti na diploma, sifa za kujiunga ni kama ifuatavyo:
- Ngazi ya Cheti (NTA Level 4): Waombaji wanapaswa kuwa na angalau ufaulu wa masomo manne (4) katika mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) kwa alama ya ‘D’ au zaidi. Masomo ya dini hayatazingatiwa.
- Ngazi ya Diploma (NTA Level 5): Waombaji wanapaswa kuwa na ufaulu wa angalau alama moja ya ‘Principal Pass’ na moja ya ‘Subsidiary’ katika mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) au cheti cha NTA Level 4 kutoka taasisi inayotambulika na serikali. Pia, wanapaswa kuwa na ufaulu wa masomo manne (4) katika mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE), bila kujumuisha masomo ya dini.
Kujua sifa za kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI) ni hatua muhimu kwa waombaji wanaotaka kujiunga na chuo hiki kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Ni vyema waombaji kuhakikisha wanakidhi vigezo vilivyowekwa na chuo ili kuongeza nafasi zao za kufanikiwa katika mchakato wa udahili. Kwa maelezo zaidi na mwongozo wa kina, waombaji wanashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya LGTI au kuwasiliana moja kwa moja na ofisi ya udahili ya chuo.