Table of Contents
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (National Institute of Transport – NIT) ni taasisi ya elimu ya juu inayotoa mafunzo katika nyanja za usafirishaji, uhandisi, teknolojia, na masuala ya biashara. Kikiwa chini ya Wizara ya Uchukuzi, NIT imeendelea kukua na kuimarika katika kutoa mafunzo yenye ubora wa hali ya juu kwa ngazi mbalimbali za elimu, kuanzia cheti, diploma, shahada, hadi shahada za uzamili.
Katika mwaka wa masomo wa 2025/2026, NIT inaendelea kuboresha viwango vya elimu kwa kufuata miongozo ya udahili inayohakikisha waombaji wanakidhi vigezo stahiki.
Umuhimu wa sifa za kujiunga ni kuweka viwango vinavyohakikisha kwamba wanafunzi wanaohitajika wana ujuzi na maarifa ya msingi yaliyo muhimu kwa mafanikio katika programu zao za masomo.
1 Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Shahada ya Kwanza
Ili kujiunga na programu za shahada ya kwanza NIT, waombaji wanahitajika kuwa na angalau ufaulu wa kuanzia daraja la pili katika masomo ya kiwango cha ‘A-Level’. Waombaji wanaweza kupitia mwongozo wa TCU kwa orodha kamili ya programu na sifa za kiingilio.
Sifa na Vigezo vya Jumla kwa Kwa waombaji wa kidato cha sita (General Minimum Entry Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kabla ya 2014 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
2 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita mnamo 2014 na 2015 | Passi mbili kuu (‘C’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 kutoka kwa masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1; E = 0.5) |
3 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kuanzia 2016 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
Sifa na Vigezo vya Jumla Kwa waombaji wa Diploma (For Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waombaji wa Stashahada ya Kawaida, FTC na Sawa | Angalau pasi nne (“D” na zaidi) katika “O” Level au NVA Level III na chini ya pasi nne “O” Level au sawa na sifa za kigeni kama ilivyothibitishwa na NECTA au NACTVET; na i) Angalau GPA ya 3.0 kwa Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6); au ii) Wastani wa alama “C” kwa Cheti cha Fundi Kamili (FTC) (ambapo A=5, B=4, C=3, na D=2); au iii) Wastani wa alama “B” kwa Stashahada ya Elimu ya Ualimu; au iv) Wastani wa alama “B” kwa tuzo zinazohusiana na Afya kama Tiba ya Kliniki na nyinginezo; au v) Alama ya Heshima kwa Stashahada na vyeti visivyofungamana na NTA; au vi) Upper Second Class kwa stashahada zisizo za NTA. |
2 | Cheti cha Msingi cha OUT | GPA ya 3.0 iliyokusanywa kutokana na masomo sita muhimu na angalau Alama ya “C” kutoka masomo matatu katika klusta husika (Sanaa, Sayansi na Masomo ya Biashara) pamoja na Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari kilicho na alama angalau 1.5 kutoka masomo mawili; au Stashahada ya Kawaida kutoka taasisi inayotambuliwa yenye GPA ya angalau 2.0 AU NTA level 5 / Cheti cha Fundi wa Kitaalam Kiwango cha II. |
Programu maalum, kama vile za afya, zinaweza kuhitaji vigezo zaidi kama vile alama za D katika masomo ya sayansi.
2 Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Uzamili na Uzamivu
Mahitaji kwa programu za uzamili na uzamivu NIT yanategemea awe na shahada ya kwanza yenye ufaulu wa kutosha, kawaida ni GPA ya 2.7 na juu, na uzoefu wa kazi kwa baadhi ya programu maalum. Kwa waombaji wa PhD, machapisho na utafiti vinaweza kuhitajika.
Sifa na vigezo vya Kujiunga kwa Programu Zote
S/N | Kuingia katika | Sifa za Kuingia |
1 | Programu ya Cheti cha Uzamili | Angalau Shahada ya Kwanza (UQF level 8). |
2 | Programu ya Stashahada ya Uzamili | Cheti cha Uzamili AU Shahada ya Kwanza (UQF level 8) yenye GPA ya angalau 2.0 au alama ya C. |
3 | Programu ya Shahada ya Uzamili (aina zote) | a) Shahada ya Kwanza ya Kitaaluma inayofaa (UQF level 8) au sawa na hiyo yenye GPA ya 2.7 au alama ya B; b) Stashahada ya Uzamili katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B; au c) Sifa ya mafunzo ya kitaalam yenye mafunzo ya ziada yanayofaa, ushahidi wa uwezo wa utafiti na uzoefu wa kazi unaofaa. |
4 | Programu ya PhD (aina zote) | Shahada ya Uzamili (UQF level 9) katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B. |
3 Mchakato wa Maombi na Tarehe Muhimu
Hatua za Kuomba
- Maombi ya mtandaoni: Waombaji wanatakiwa kujaza fomu za maombi mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya NIT.
- Ada za maombi: Kiasi hiki kinaweza kulipwa kupitia benki zilizoidhinishwa au mkondoni.
- Tarehe za mwisho: Tarehe maalum za mwisho za maombi na usaili lazima zifuatwe ili kuepuka kuchelewa.
Sifa za kujiunga na NIT zimeundwa kuhakikisha wanafunzi wana ‘background’ thabiti kuwawezesha kufanikiwa katika masomo yao. Ni muhimu kwa waombaji kuchukua muda kujiandaa ipasavyo ili kukidhi vigezo vya udahili. Usikose kutumia mwongozo wa TCU na tovuti ya NIT ili kuhakiki taarifa zenye usahihi zaidi na kujiandaa kwa usaili vizuri.
Kwa maelezo zaidi na mwongozo wa maombi, tembelea TCU Guidebook.