zoteforum.com
No Result
View All Result
  • Login
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
PRICING
JIUNGE
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
No Result
View All Result
zoteforum.com
No Result
View All Result

TCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA 2025/2026

TAARIFA KWA UMMA KUKAMILIKA KWA AWAMU YA KWANZA NA KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

KUKAMILIKA KWA AWAMU YA KWANZA YA UDAHILI 2025/2026

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika. Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yanatangazwa na vyuo husika.
Katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 146,879 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 88 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika Shahada ya Kwanza. Aidha, jumla ya programu 894 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 856 mwaka 2024/2025, ikiwa ni ongezeko la programu 38 za masomo. Vilevile kwa upande wa nafasi za udahili, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 205,652 ikilinganishwa na nafasi 198,986 mwaka uliopita. Hili ni ongezeko la nafasi 6,666 sawa na asilimia 3.3 katika programu za Shahada ya Kwanza.
Pia katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 116,596 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji wote walioomba udahili, wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba. Idadi ya waombaji wa udahili na watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika Awamu ya Pili ya udahili.

WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025. Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI 2025/2026

Tume inatangaza kuwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imeanza leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025. Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.
Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi. Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI

Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika. Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

ADVERTISEMENT

Usikose Kusoma na Hizi Pia

VITUO VYA USAILI WA MAHOJANO WA MDAs & LGAs UTAKAOFANYIKA TAREHE 22 HADI 24 OKTOBA, 2025

Serikali yatangaza Nafasi za Kazi za ualimu (10,026)

Nafasi za kazi Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II)

Nafasi za kazi Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daro la II

Nafasi za kazi MSANIFU MAJENGO DARAJA LA II (ARCHITECT GRADE II)

Nafasi za kazi Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Daraja la II (Aquaculture Officer Grade II)

Nafasi za kazi FUNDI SANIFU DARAJA LA II – KILIMO (AGRICULTURAL TECHNICIAN GRADE II)

Nafasi za kazi Mkufunzi DARAJA LA II – Kilimo (Agricultural Officer Grade II)

Nafasi za kazi Afisa Kilimo Msaidizi DARAJA LA III (Agricultural Field Officers)

Nafasi za kazi Afisa Kilimo Msaidizi DARAJA LA II (Agricultural Field Officers)

Load More
SendShareShareTweet
Zoteforum

Zoteforum

Karibu Zoteforum.com, Tovuti yako pekee inayokupasha habari na Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani.

Makala Nyingine zaidi

Nafasi za kazi Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Nafasi za kazi Afisa Kilimo Msaidizi DARAJA LA III (Agricultural Field Officers)

Nafasi za kazi Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Nafasi za kazi Afisa Hesabu DARAJA LA II (Accounts Officer II)

TCU Multiple Selection 2025/2026 – Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo Vikuu/Chuo Zaidi ya kiMoja au Programu Zaidi ya Moja

Orodha ya Waombaji ambao hawajathibitisha udahili katika awamu ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo Vikuu 2025/2026 (University and colleges Selection/ selected/applicants)

Orodha ya Waombaji Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja katika Awamu ya Pili (2025/2026)

Load More

Weka maoni yako hapa au Komenti kuhusu makala hiiCancel reply

  • About
  • Cart
  • Checkout
  • Contact
  • Download Mziki na Nyimbo mpya
  • Habari za Burudani
  • Habari za Elimu
  • Habari za Soka
  • Home
  • Matokeo Ya Mitihani Tanzania – NECTA – MOCK – VYUO
  • My account
  • Nafasi za Kazi 2024
  • Offerings
  • Shop
  • Subscription
Call us: +1 234 JEG THEME

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.