VETA Arusha ni miongoni mwa vyuo maarufu vya ufundi nchini Tanzania, kikilenga kuwapatia wanafunzi ujuzi wa vitendo unaohitajika kwenye soko la ajira. Lengo kuu la chuo hiki ni kutoa mafunzo yenye tija ambayo huwasaidia wahitimu kweny ushindani katika soko la ajira na hata kujiajiri wenyewe.
Chuo cha VETA Arusha kipo mkoani Arusha, na kinatoa kozi mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira sambamba na kutoa nafasi kwa wahitimu wake kuzalisha ajira kupitia stadi walizopata. Kozi hizi zinawezesha vijana wengi kupata elimu stahiki na ujuzi wa kutosha kukabiliana na changamoto za kiuchumi na ajira. Ujuzi huu unachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi kwa kuongeza idadi ya wataalamu stadi.
Katika makala hii tumechambua kozi zinazotolewa na Chuo cha Ufundi Stadi VETA Arusha, gharama zake, pamoja na namna ya kujiunga kwako kwa mwaka wa masomo wa 2025.
Orodha ya Kozi Zinazotolewa na Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Arusha na Ada zake
Chuo cha VETA Arusha kinatoa kozi kadha wa kadha zinazogusa nyanja mbalimbali za ufundi stadi. Zifuatazo Hapo chini ni orodha ya kozi zinazotolewa na ada zake kwa mwaka wa 2025:
NA | JINA LA FANI | MUDA | ADA | BWENI | KUTWA |
1 | Udereva wa Magari ya Abiria (Passenger Service Vehicle – PSV) | Wiki 2 | 222,000 | – | – |
2 | Udereva wa Magari (VIP-Daraja la 2) | Wiki 2 | 325,000 | – | – |
3 | Udereva wa Magari (VIP- Daraja la 1) | Wiki 2 | 360,000 | – | – |
4 | Udereva wa Awali (Basic driving of Motor Vehicle) | Wiki 5 | 217,000 | – | – |
5 | Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fittings) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
6 | Ushonaji (Designing Sewing and cloth technology) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
7 | Umeme wa Majumbani (Electrical Installation) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
8 | Uungaji Vyuma (Welding and metal fabrication) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
9 | Ujenzi (Masonry and Brick laying) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
10 | Useremala (Carpentry and joinery) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
11 | Zana za Kilimo (Agro mechanics) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
12 | Ufundi wa magari (Motor Vehicle Mechanics) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
13 | Ufundi Umeme wa Magari (Auto Electric) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
14 | Kompyuta (Computer Application) | Miezi 3 | 240,000 | 460,000 | – |
Kozi hizi zinalenga kukuandaa kwa ujuzi wa kina katika fani husika, kukuwezesha kuwa mbunifu na mwenye uwezo wa kutatua changamoto za kiufundi.
Utaratibu wa Jinsi ya Kujiunga na Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Arusha kwa Mwaka 2025
Ikiwa unapenda kujiunga na kozi yoyote kati ya zilizoorodheshwa hapo juu, unapaswa kufahamu utaratibu wa kujiunga na chuo hiki kwa mwaka 2025.
Kujiunga na chuo cha VETA Arusha, utahitajika kujaza fomu ya maombi ambayo inapatikana kwa gharama ya Tsh 5,000/=. Unaweza kutembelea moja kwa moja ofisini kwao au walisiana na kupitia mawasiliano yaliyotolewa ili upate maelezo zaidi pamoja na Control Number kwa ajli ya malipo.
Mawasiliano ya chuo ni kama ifuatavyo:
- Namba ya simu: 0736 500 507
- Barua pepe: arushavtc@veta.go.tz
Hakikisha unachukua hatua hizi ili kupata nafasi yako mapema na kujihakikishia nafasi ya kuwa miongoni mwa wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na VETA Arusha.
Kwa maelezo zaidi juu ya jinsi ya kujisajili na kupata fomu za kujiunga na chuo hiki, unaweza kutembelea mwongozo wa kozi za muda mfupi za VETA kwa mwaka 2025 kupitia linki hii: Mwongozo wa Kozi za Muda Mfupi VETA 2025.
Hitimisho
Kwa kumalizia, VETA Arusha imeendelea kuboresha hali ya elimu na mafunzo ya ufundi kwa kutoa ujuzi na maarifa yanayohitajika katika soko la ajira. Kuanzia kozi za udereva, ufundi bomba, umeme, useremala hadi zana za kilimo na zaidi, chuo hiki kinatoa chaguo pana kwa wanafunzi wa ufundi stadi.
Ikiwa umepanga kujiunga na chuo hiki, hakikisha unafuata utaratibu uliotolewa wa kupata fomu za kujiunga. Endapo una maswali au unahitaji maelezo zaidi, chuo kimeweka namba za mawasiliano pamoja na barua pepe ambapo unaweza kupata msaada zaidi. Asante kwa kuzindua makala hii, na tunakutakia mafanikio katika safari yako ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi.