Nafasi 50 za Madereva
Kampuni ya Unique Consultancy Services Co. Ltd inatangaza nafasi 50 za madereva wa matrekta, mabasi makubwa, mabasi madogo, pikapu, magari ya kubeba maji, matanki ya mafuta, malori na waendeshaji crane katika mradi uliopo kwenye maeneo ya Tanga, Kagera, Geita na Tabora.
Sifa za Mwombaji
- Lazima awe na uelewa mzuri wa sheria za usalama barabarani na aweze kuzitafsiri.
- Lazima asiwe na umri chini ya miaka 25 na asiwe zaidi ya miaka 45.
- Lazima awe na leseni halali ya kuendesha chombo husika na isiyokuwa imeisha muda wake.
- Lazima awe amehudhuria mafunzo ya ufundi stadi na kupata cheti kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali.
- Lazima awe tayari kwenda na kufanya kazi katika maeneo ya mradi, chakula na malazi yatatolewa bila malipo.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao kupitia baruapepe uccjobs2025@gmail.com kabla ya tarehe 15 Juni 2025, wakiambatanisha wasifu wao (CV) na nyaraka nyingine zote kwenye mfumo wa pdf, zote kwa pamoja.