TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Utangulizi
Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo:
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI NNE (04)
1.1 Majukumu ya Kazi
i. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala mwenye regista (Incoming Correspondence Register) ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register) iii. Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers) iv. Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji v. Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa vi. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
1.2 Sifa za Mwombaji
- Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
- Kuwa na ujuzi wa Kompyuta
1.3 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI TATU (03)
2.1 Majukumu ya Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali vi. Kufanya usafi wa Gari vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
2.2 Sifa za Mwombaji
- Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Kuwa na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali
- Kuwa na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika
- Kuwa wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
2.3 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ni TGS B
3.0 Masharti ya Jumla
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne na cha Sita, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards))
v. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAYATAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET)
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
viii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walio katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010
x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria
xi. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) ilyosajiliwa na Wizara ya Ardhi xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 Agosti, 2025
xiii. Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoonwa “Recruitment Portal”)
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
Taarifa za Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua S.L.P 83 KALIUA
Simu: +255 262 965 679, +255 262 965 676, +255 622 225 618 Barua pepe: ded@kaliuadc.go.tz Tovuti: www.kaliuadc.go.tz
Mkurugenzi Mtendaji (W)
KALIUA, TABORA
DOWNLOAD: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA 01-08-2025