Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza ratiba ya Mtihani wa kidato cha sita 2025 unaotarajiwa kuanza tarehe 05/05/2025. Mtihani wa huu ni muhimu kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na elimu ya juu nchini.
Ratiba ya mtihani wa kidato cha sita ni mpangilio wa tarehe, muda na masomo yanayotarajiwa kufanywa na wanafunzi wa kidato cha sita katika mitihani yao ya mwisho ya kiadato cha sita 2025. Ratiba hii Inatoa mwongozo wa jinsi mitihani ya nadharia na vitendo itakavyofanyika katika kipindi kilichopangwa. Ratiba hiyo inajumuisha masomo mbalimbali na vipindi tofauti vya mitihani ambavyo huratibiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kujua ni lini na wapi watafanya kila somo la mtihani wao.
Ratiba hii ni muhimu kwa maandalizi na utendaji bora katika mitihani, kwani inaelezea ni lini kila mtihani utafanyika, kwa hivyo wanafunzi wanaweza kupanga muda wao na kujiandaa ipasavyo kabla ya mitihani.


Ratiba ya mtihani wa kidaato cha sita 2025 imegawanyika kwa siku tofauti. Siku ya Jumatatu ya tarehe 5 Mei 2025, kutakuwa na mtihani wa General Studies kuanzia saa nane kamili hadi saa kumi na moja jioni. Baadaye siku hiyo hiyo, mtihani wa Lugha ya Kiswahili 1, Kemia 1, na Uchumi 1 utaanza saa nane hadi saa kumi na moja jioni.
Jumanne, tarehe 6 Mei 2025, masomo kama Kiswahili 1, Basic Applied Mathematics, pamoja na Advanced Mathematics 1 yataanza saa moja asubuhi hadi saa nne asubuhi, huku masomo kama Historia 1, Lugha ya Kichina 1, Biolojia 1, na Uhasibu 1 yakiwa yanaendelea mchana kuanzia saa nane hadi saa kumi na moja.
Jumatano tarehe 7 Mei 2025, kutakuwa na mtihani wa Kiswahili 2, Fizikia 1, Kilimo 1, Biashara 1, na Lishe ya Binadamu 1 asubuhi kuanzia saa moja hadi saa nne asubuhi. Mchana utafuatwa na mitihani ya Jiografia 1, Elimu ya Michezo 1, Lugha ya Kifaransa 1, na masomo ya Elimu kuanzia saa nane hadi saa kumi na moja jioni.
Siku ya Alhamisi, tarehe 8 Mei 2025, kutakuwa na mtihani wa Historia 2 na Biolojia 2 asubuhi, na mchana kutakuwa na mitihani ya Lugha ya Kiingereza 2, Kemia 2, pamoja na Biashara 2. Hii itaendelea hadi Ijumaa tarehe 9 Mei 2025 ambapo kutakuwa na mitihani ya masomo mbalimbali na kumalizia na Sanaa 1, Lugha ya Kichina 2, Fizikia 2, na Uchumi 2 mchana.
Mbali na mitihani ya nadharia, ratiba hii pia ina vipimo vya vitendo kwa baadhi ya masomo kama vile Biolojia, Kemia, na Fizikia. Vipimo hivi vya vitendo vinapaswa kutazamwa kwa umuhimu mkubwa vilevile vitafanya sehemu kubwa ya alama zako za mwisho.
Ni vizuri kuhakikisha unatambua ni lini na wapi vipimo vinafanyika ili uweze kufika wakati sahihi bila haraka haraka zisizo za lazima. Hii ni muhimu kwa sababu vipimo vya vitendo vinaweza kuwa na namna tofauti za uandaaji, kulinganisha na mitihani ya nadharia. Kwa mfano, somo la Kemia linayo Practical Chemistry 3A, 3B, na 3C kuanzia tarehe 14 hadi 26 Mei 2025, na hivyo ni muhimu kufuatilia ratiba ya kila siku.
Kufahamu zaidi na kujionea mwenyewe kwa ajili ya kumbukumbu zako na maandalizi ya mtihani wako wa kidato cha sita unaweza kupakua Ratiba ya matihani wa kidato cha Sita kupitia linki hapo chini:
DOWNLOAD NECTA ACSEE 2025 EXAM TIMETABLE – RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025