Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Oktoba 24,2025 imetoa awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 135,240. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatato:
i. Wanafunzi 40,952 wa shahada ya awali na wanafunzi 5,342 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 152 bilioni.
ii. Wanafunzi 615 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 3.3 bilioni.
iii. Wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mkopo kiasi cha TZS. 271.2 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.
Bodi ya Mikopo itaendelea kutoa awamu zingine za mikopo na skolashipu kadiri itakavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Aidha, Bodi ya Mikopo inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.
Bofya hapa kujua kama umepata mkopo
Check Your HESLB loan allocation status here
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Ijumaa, Oktoba 24, 2025


Tunashukuru kwa waliopata mkopo,tunaomba waliofanya marekebisho nao wafikiriwe kabla ya vyuo kufunguliwa
Msaada nahitaji kujua kwanini ,nikingia kwenye account ya ndugu yangu ili kuona kama ni mnufaika wa mkopo preview application status haifunguki?
jamani fanyeni haraka wengine bila mkopo chuo tutapasikia tu hali mbaya
Ivi kwanini Mimi kama privet candidate nimetengwa na ni miongoni mwa wanafunzi waliotuma maombi yangu mapema ila niliotuma nao wao wamepata Mimi nikaachwa Kuna ubaguzi apo tazameni hili, private wenginine tumepambana sana na wazazi hawana kitu hapa tulipofikia na tunapohitaji msaada wa serekali tunabaguliwa kwanini na kwanini tuwekwe kwenye second na tulitupa first hili sio sawa Mimi kama Mimi nikikosa hapa ndo mwisho wangu wa elimu unafikiri najiskiaje alafu natazama television naona watu wananunua magoli Kwa million Tano na mimi nipo mtaani baada ya kukosa mkopo ivi au ni Kwa vile mimi ni private? Apana ili sio sawa MUNGU anawaona maana documents zote mlizo hitaji nimewasilisha kwenu mbona natupwa kama second chance na wakat nilikua first kwenye kutuma maombi yangu kwanini mpo hivyo nyie body ya mkopo?
Kitu muhim ni mkopo tu kwangu bila mkopo basi elimu yangu ndyo hatima yake hii tusaidieni pale mnapoweza tupate mkopo.
kwakweli jamani tumejinyima sana hadi kuomba mkopo
mimi nimekosa mkopo sijui ntasomaje hata kama kama nilisoma private ni miaka miwili tu na ni olevel hamuwezi jua nilisomeshwaje mpaka nafikia hatua nakata tamaa kabisa nimeomba mwanzoni nimetumia gharama kubwa Leo hii nasubiria round ya pili nalelewa na single mother sijui itakuwa Sina uhakika wakupata second round hata sipa tu bado mtuonee huruma tuna ndoto kubwa hapo baadae tuna wazazi na ndugu wanatutegemeaMungu atusaidie daah inaumiza sana
msichoke kutufikiria tuliokosa tutapoteza ndoto zetu nyingi
Wengine sisi so watanzania Hadi tunaomba mkopo mala mbilimbili hatupati