Mchakato wa form five selection au uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya kati ni tukio muhimu linalotoa nafasi kwa wanafunzi kuendelea na masomo yao ya juu zaidi baada ya kuhitimu kidato cha nne. Mkoa wa Pwani una historia ya kushikilia nafasi muhimu katika utoaji wa elimu nchini Tanzania. Pwani ni miongoni mwa mikoa inayokua kwa kasi na inayoelekeza nguvu katika kuboresha miundombinu ya shule na vyuo kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo.
Katika kipindi cha mwaka 2025, mchakato wa uchaguzi ulifanyika kupitia mfumo wa SELEFORM, ambao umetoa nafasi kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kubadilisha machaguo ya tahasusi za Kidato cha Tano na kozi za vyuo mbalimbali. Mfumo huu unaojulikana kama selform umewawezesha wanafunzi kuona na kuchagua fursa ambazo zinaendana na matarajio yao ya baadaye na hatimaye majina ya waliochaguliwa kidato cha tano mkoani Pwani yataweza kupatikana na kutangazwa kupitia tovuti ya TAMISEMI.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, Katika Mkoa wa Pwani
Kwa wale ambao walituma maoombi ya kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya kati kupitia mfumo wa selform, ni muhimu kufahamu namna ya kuangalia majina yao kama wamechaguliwa kwa jili ya kuanza maandalizi kwa wakati. Orodha ya waliochaguliwa kidato cha tano na kuingia katika vyuo vya kati inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (www.nactvet.go.tz). Vilevile, unaweza kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi kwa kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Hatua za kuangalia majina ya waliochaguliwa ni pamoja na:
- Ingia kwenye tovuti ya TAMISEMI (https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/).
- Fuata link ya ‘Form Five First Selection, 2025’.
- Chagua orodha ya mikoa na kisha chagua mkoa wa Pwani.
- Chagua halmashauri husika na kufungua shule uliyosoma.
- Angalia orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka shule husika na kupata maelekezo ya kujiunga.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Pwani
Uchaguzi huu unafanyika kwa ngazi ya wilaya na unazingatia shule zilizopo katika mkoa wa Pwani. Kuona matokeo ya Form five selection moja kwa moja na kwa urahisi zaidi bila usumbufu unaweza kutumia linki zifuatazo hapo chini.
CHAGUA HALMASHAURI
Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Pwani
Ili kupata maelekezo sahihi kuhusu jinsi ya kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya elimu ya ufundi kwa waliochaguliwa katika mkoa wa Pwani, unahitajika kutembelea tovuti ya TAMISEMI. Angalia sehemu ya ‘UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025’ , Bofya link ya jina la shule au chuo ulichochaguliwa ili kupakua maelekezo ya kujiunga.
Kwa kufuata hatua hizo, utakaribishwa na taarifa muhimu zenye maelekezo ya kina ambayo yanakuhusu wewe kama mmoja wa waliochaguliwa kidato cha tano mwaka 2025 katika mkoa wa Pwani. Furahia safari yako mpya ya elimu na hakikisha unaandaa mahitaji yote muhimu kabla ya kuanza shule au chuo.