Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza rasmi orodha ya majina ya wahitimu wa kidato cha sita 2025 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025, hatua ambayo inatazamwa na wengi kama sehemu muhimu ya mchakato wa malezi, ujenzi wa uzalendo, na maandalizi ya vijana wa Kitanzania kwa ajili ya maisha na maendeleo ya taifa. Tangazo hili limekuja mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchambuzi wa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2025, ambapo vijana kutoka shule tofauti za Tanzania wamepangiwa katika makambi mbalimbali nchini kwaajili ya mafunzo haya muhimu.
Orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa tayari ipo kwenye tovuti rasmi ya JKT, ambayo ni www.jkt.go.tz, na kwamba majina haya yanaweza kupatikana kwa kupakua faili lenye orodha kamili au kutumia mfumo wa kanzidata maalum ambapo mwanafunzi atalazimika kuingiza taarifa zake binafsi kama vile namba ya shule, majina kamili na taarifa nyingine zinazohitajika ili kuweza kupata majibu endapo amepata nafasi au la. Mfumo huu umerahisishwa ili kumwezesha kila mmoja kupata matokeo haraka na bila usumbufu.



Jinsi ya Kuangalia Majina ya form six Waliochaguliwa JKT 2025 (Mujibu wa sheria)
Mara baada ya kutangazwa rasmi na JKT, Orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa itapatikana kupitia njia kuu zifuatazo:
Kupitia Linki ya moja kwa moja
Kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) kwa njia ya linki ya moja kwa moja (direct link) bofya linki ifuatayo:
- Majina ya form six (kidato cha sita 2025) Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mwaka 2025 (mujibu wa sheria)
- form six Waliochaguliwa JKT 2025 (Mujibu wa sheria)
Kupitia Tovuti Rasmi ya JKT
Hatua hizi zimepangwa ili kukuwezesha kupata orodha kamili na ya uhakika:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya JKT:
- Nenda kwenye kivinjari chako (browser) na andika www.jkt.go.tz.
- Tafuta Sehemu ya “Matangazo” au “Habari Mpya”:
- Kwa kawaida, “Matangazo” au “Notice Board” hupatikana kwenye ukurasa wa mbele au menyu kuu ya tovuti.
- Chagua Kiungo cha “Majina ya form six Waliochaguliwa JKT 2025”:
- Bonyeza kiungo husika kilichoandikwa “Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025” au maneno yanayofanana.
- Pakua Orodha ya Majina (PDF Download):
- Mara nyingi, orodha hii hupakiwa katika mfumo wa PDF. Bonyeza kiungo cha kupakua na hifadhi faili.
- Tafuta Jina Lako:
- Tumia amri ya kutafuta (Ctrl + F kwa Windows au Command + F kwa Mac) na andika jina lako au namba ya mtihani ili kupata jina lako haraka kwenye listi ndefu.
Vidokezo Muhimu:
- Hakikisha unaangalia tangazo la mwaka husika (2025) kwani matangazo ya miaka iliyopita yanaweza kuwa bado mtandaoni.
- Hifadhi nakala ya orodha hiyo kama ushahidi na marejeo ya baadaye.
Kupitia Kanzidata Maalum ya JKT (Online Database)
JKT imeanzisha mfumo wa mtandaoni unaorahisisha mchakato wa kuangalia majina na kambi ulipopangiwa:
- Tembelea www.jkt.go.tz na chagua sehemu ya kanzidata ya waliochaguliwa.
- Jaza taarifa zako (namba ya shule, jina la kwanza, jina la kati, jina la mwisho — kama ilivyo kwenye vyeti vyako).
- Bonyeza “Tafuta” na subiri mfumo uonyeshe majina na kambi uliyopangiwa.
Angalizo: Ikiwa huoni jina lako, hakikisha umepata matokeo ya mwaka sahihi na umejaza taarifa zako kwa usahihi.
Maandalizi kwa Waliochaguliwa na Vifaa Muhimu
Kabla ya kuripoti kambini, wahitimu wanapaswa kujitayarisha kisaikolojia na kimtindo kidogo kwa kuhakikisha wanakuwa na vifaa muhimu kama ifuatavyo:
Orodha ya Vifaa Muhimu:
- Bukta ya Dark Blue (spesho kwa wanawake)
- T-shirt ya kijani isiyoandikwa (Green Vest)
- Raba za michezo (kijani/bluu)
- Shuka mbili rangi blue bahari
- Soksi ndefu za rangi nyeusi
- Nguo za baridi (kama sweta/koti)
- Track suit ya kijani au bluu
- Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu (kidato cha nne na sita), kitambulisho cha taifa/NIDA
- Nauli kwenda na kurudi kambini
- Mengine muhimu kama afya/mahitaji binafsi
Vidokezo vya Kujiandaa:
- Hakikisha una vifaa vyote kabla ya safari.
- Jitayarishe kisaikolojia — mafunzo ya JKT yanahitaji subira, nidhamu, na ushirikiano.
- Weka nakala za nyaraka zako muhimu sehemu salama.
Je ni hupo utaratibu kwa vijana ambao wamemaliza kidato cha sita lakin awajachagiliwa kujiunga na mafunzo lakin wanawiwa kujiunga na mafunzo hayo
Ndyo wapo
Mimi naitwa pius Bhoke Wambura sijachaguliwa ila nina wiwa kwenda nafanyaje naomba msaada natoka Mara secondary.SO129.au nijulisheni kwa namba 0679876016
Kwa wale ambao hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kwenda jkt n wanataka kwenda wanatakiwa kufuata utaratibu gani? Naomba msaada kupitia namba hii 0787977795