Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Oktoba 24,2025 imetoa awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 135,240. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatato:
i. Wanafunzi 40,952 wa shahada ya awali na wanafunzi 5,342 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 152 bilioni.
ii. Wanafunzi 615 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 3.3 bilioni.
iii. Wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mkopo kiasi cha TZS. 271.2 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.
Bodi ya Mikopo itaendelea kutoa awamu zingine za mikopo na skolashipu kadiri itakavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Aidha, Bodi ya Mikopo inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.
Bofya hapa kujua kama umepata mkopo
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Ijumaa, Oktoba 24, 2025

