Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa kuzingatia kibali cha Ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kumb Na. FA.9787/288/01/09 pamoja na vibali vya Ajira mbadala Kumb.Na. FA.228/613/01/D’/029 ya tarehe 27.06.2024 na Kumb.Na. FA.228/613/01/D’/061 cha tarehe 09.07.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu OR-UTUMISHI, Anarudia kuwatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa ya kuomba nafasi za kazi sita (6) kama inavyoonekana hapo chini:
1.0 DEREVA DARAJA LA II NAFASI (04)
- MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.2 MSHAHARA; TGS ‘B’
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II NAFASI – (02)
- MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
- Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada au nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi na;
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.3 MSHAHARA TGS ‘C’
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Certificates,- Cheti cha mtihani wa kidato cha IVnaVI,-Computer Certificate,-
Vyeti vya Kitaaluma
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTAna NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushiwa husika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 30/11/2024.
- MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na Vyeti vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P 16, TARIME.
- Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira (RecruitmentPortal) kupitia anuani ifuatayo:https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal“).
xv. Maombi yatakayo wasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
Imetolewa na
MKURUGENZI MTENDAJI (W) TARIME