Tangazo la kazi ya Afisa Uvuvi Msaidizi DARAJA LA II (Assistant Fisheries Officer II)
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 35 za Afisa Uvuvi Msaidizi DARAJA LA II (Assistant Fisheries Officer II) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi. ii. Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki. iii. Kutega mitego Ziwani au Baharini. iv. Kutengeneza nyavu ndogo ndogo. v. Kuwapa chakula samaki katika mabwawa. vi. Kuvua samaki katika mabwawa. vii. Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi. viii. Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki. ix. Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na samaki. x. Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya kuzingatia.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) katika fani za Sayansi ya Uvuvi (Fisheries Science/Management, Zoology, Microbiology, Marine Biology, Food Science and Aquaculture) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
TGS.C
MASHARTI YA JUMLA NA JINSI YA KUTUMA MAOMBI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.