Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepata kibali cha Ajira Mpya kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 3)
1.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari. ii. Kuwapeleka watumishi sehemu mbalimbali kwenye safari za kikazi. iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari. iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali. v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari. vi. Kufanya usafi wa gari, na vii. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Kidato cha nne (Form IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne (IV).
- Awe na Leseni ya Daraja la ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji magari pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
- Awe pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyoonyesha sifa ya kupata madaraja husika.
- Awe ameenda mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni TGS B.
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu kwenye mfumo wa kuombea ajira kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CCA. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
v. Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili (Diploma/Certificate, cheti kidato cha nne/sita, mafunzo mbalimbali, Certificate cha Computer, vyeti vya kitaaluma).
vi. Hati ya Testimonials, “Provision Results”, “Statements Results”, na matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWI.
vii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.
x. Waombaji wenye majina tofauti katika vyeti vya taaluma, kuzaliwa na NIDA waambatane DEED POLL (Hati ya Usajili wa Kiapo cha Majina).
xi. Waombaji wenye utofauti wa herufi kati ya kitambulisho cha Taifa na vyeti vya taaluma, kidato cha nne na cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kuambatisha AFFIDAVIT (Kiapo).
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/08/2025.
xiii. MUHIMU: Kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya maombi ielekezwe kwa: Mkurugenzi wa Manispaa, Manispaa ya Kigoma Ujiji, S.L.P 44, KIGOMA.
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ xv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na,
Kisena M. Mabuba MKURUGENZI WA MANISPAA KIGOMA/UJIJI