Halmashauri ya Wilaya ya Makete kupitia Kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 chenye kada ya Dereva Daraja la II nafasi (12) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete anawatangazia nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wote wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ilivyoainishwa hapa chini:
1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 12
1.1.1 Kazi / Majukumu ya Dereva Daraja la II
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari, ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi, iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari, iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali, v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari, vi. Kufanya usafi wa gari, vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake, viii. Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
2.1.2 Sifa za Mwombaji
- Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
- Pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.1.3 Ngazi ya Mshahara
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B1
Masharti ya Jumla
i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 hadi isiyozidi miaka 45. ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwa mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. iii. Waombaji wote waambilishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ikiwemo vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates
- Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI
- Cheti cha Kompyuta (Computer Certificate)
- Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards) v. “Testimonial”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (Form IV and Form VI Results Slips) HAYATAKUBALIWA. vi. Waombaji wa kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo ya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. vii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07/08/2025. xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete S.L.P. 6 MAKETE
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na: Ligobert W. Kalisa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete