Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imekamilisha Awamu ya kwanza ya udahili wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027. Katika awamu hii, waombaji wengi wamepata udahili katika vyuo mbalimbali, huku baadhi yao wakichaguliwa katika zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja. Hali hii inahitaji waombaji kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee ili kuruhusu mchakato wa udahili kuendelea kwa ufanisi. Kuangalia Majina ya Waombaji Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja au Programu Zaidi ya Moja katika Awamu ya kwanza bofya linki hapo chini
Orodha ya Waombaji ambao hawajathibitisha udahili katika awamu ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/27
Ni muhimu kwa waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee ndani ya muda uliopangwa.

