Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), MDAs & LGAs, Wizara ya Afya, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 06-08-2025 hadi 26-08-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
Maelekezo ya Usaili
1. Tarehe, Muda na Sehemu ya Usaili
Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Udhibitisho wa Kuwasilisha
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
3. Vitambulisho Vinavyokubalika
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Leseni ya Udereva
- Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka
4. Vyeti Vinavyotakiwa
Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Kidato cha IV, Kidato cha VI
- Astashahada
- Stashahada
- Stashahada ya Juu
- Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
5. Vyeti Ambavyo HAVITAKUBALIWA
Wasailiwa watakaowasilisha:
- Testimonials
- Provisional Results
- Statement of Results
- Matokeo ya Kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
Havitakubaliwa na hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
6. Masuala ya Gharama
- Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Tarehe, Muda na Mahali
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Waombaji Waliosoma Nje ya Tanzania
- Wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika kama TCU, NACTVET au NECTA.
9. Wale Wasioitwa Katika Tangazo
Kwa waombaji kazi ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili, wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
10. Kada Zilizopaswa Kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma
Wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.
11. Udhibiti wa Namba za Mtihani
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
12. Matatizo ya Majina
Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
PAKUA ORODHA KAMILI YA MAJINA HAPA
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA MAJINA YA NYONGEZA 31-07-2025